Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: PSG wanataka pauni milioni 145 kumtoa Barcola

Chanzo cha picha, Getty Images
Paris St-Germain wanataka pauni milioni 145 kumtoa mshambuliaji wa Ufaransa, Bradley Barcola mwenye umri wa miaka 23, huku Arsenal na Liverpool wakimtaka. (Times)
Arsenal hawajaanza mazungumzo kuhusu kumsajili mshambuliaji wa Brazil, Vinicius Jr, lakini Real Madrid wameweka bei ya euro milioni 160 (£137m) kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu huu wa joto. (Sport)
Arsenal iko tayari kumpa Vinicius mkataba mkubwa zaidi katika historia ya klabu hiyo. (Mirror)
Kipaumbele cha Vinicius ni kusaini mkataba mpya na Real Madrid. Ana mwaka mmoja uliobaki kwenye mkataba wake. (AS)
Arsenal wako tayari kuharakisha mazungumzo kuhusu kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle, Mbrazili, Bruno Guimaraes, mwenye umri wa miaka 28. (TalkSport)
Guimaraes amewaambia mawakala wake kwamba anataka mustakabali wake utatuliwe wiki ijayo, kabla ya kurejea kwenye kambi ya mazoezi ya Newcastle kabla ya msimu kuanza. (TeamTalk)
Tottenham wanapigiwa upatu kumsajili winga wa Brazil Savinho, 22, kutoka Manchester City. (Sun)
Real Madrid wamekubaliana na masharti binafsi ya winga wa RB Leipzig mwenye umri wa miaka 19, Yan Diomande. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Al-Hilal wameanza mazungumzo juu ya kumsajili winga wa Senegal, Iliman Ndiaye, 26, kutoka Everton. (Fabrizio Romano)
Chelsea itadai ada kubwa kwa winga wa Ureno, Pedro Neto, 26, huku Liverpool , Manchester City na timu za Saudi Arabia zikionyesha nia ya kumsajili. (Mail)
Besiktas wanasubiri uamuzi kutoka kwa mshambuliaji wa Misri, Mohamed Salah, 34, baada ya kuwasilisha ofa yao ya mwisho. Yeye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Liverpool. (Mail)
Bournemouth hawatarajii kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa, Junior Kroupi mwenye umri wa miaka 20, licha ya Barcelona kumtaka. (Marca)
Fulham inamtaka kiungo wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 18 Franco Mastantuono ikiwa Real Madrid itamtoa kwa mkopo msimu ujao. (AS)
Juventus wanafanyia kazi makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, 25, kutoka Manchester United. (Gazzetta dello Sport)
Kiungo wa kati wa Ureno, Joao Palhinha, 31, anataka kupigania nafasi yake Bayern Munich lakini wanataka kumuuza. (Bild)















