Mtu anayefanya 'kazi hatari zaidi duniani'

Chanzo cha picha, GETTY, NAS
Mtambo nambari 4 wa kituo cha nguvu za nyuklia cha Chernobyl nchini Ukraine uliharibiwa kabisa katika mlipuko mbaya wa Aprili 26, 1986. Lakini kwa kina cha mita 10, vituo vya udhibiti na ufuatiliaji, ambavyo vilinusurika maafa, bado viko.
"Ni kama maze kubwa chini ya kinu," Anatolii Doroshenko, 38, mtafiti katika Taasisi ya Matatizo ya Usalama wa Mimea ya Nyuklia (ISPNPP), mwanasayansi ambaye anachunguza maze ya mionzi chini ya kinu cha Chernobyl, aliiambia BBC.
Kazi yake inahusisha kuchuchunguza utendakazi wa mitambo hii walau mara moja kwa mwezi, mchakato ambao, kulingana na gazeti la New Scientist, "inaweza kuchukuliwa kuwa kazi hatari zaidi duniani."
Katika mtandao huu wa vyumba vya chini ya ardhi, kila kitu kinachafuliwa na mionzi: sakafu, vifaa, kuta na hewa.
Huko, Doroshenko ana jukumu la kudhibiti vifaa, kukusanya data, kufunga mita, kuchukua sampuli, na kufuatilia hali ya mafuta ya nyuklia.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika baadhi ya vyumba, kiwango cha mionzi ni cha juu sana kwamba lazima amalize kazi hizi kwa chini ya dakika nne na kuondoka mara moja.
Katika viingine, viwango vya mionzi viko juu kiasi kwamba hata hufai kukaribia.
Kazi yake ni muhimu kuhakikisha kila kitu kiko sawa kwenye mtambo husika.
Doroshenko anakubali kwamba kazi yake inazua hofu, lakini anaitumia kama mshirika.
"Hofu inakusaidia kuzingatia maagizo ili kuhakikisha kiwango cha mionzi kinadhibitiwa," alisema.
"Hapa, hatari kubwa zaidi ni kuzoea hali. Ukizoea kuogopa, unaanza kupuuza kwamba umezungukwa na mionzi. Chochote - glavu, kipande cha chuma - kinaweza kuchafuliwa, hata ikiwa hutambui."

Chanzo cha picha, Personal archives
Chini ya vifusi
Njia ambazo Doroshenko hupitia ni sehemu ya vifaa ambavyo hutumika kuendesha kinu cha nyuklia cha Chernobyl.
Ni mahali palipo na giza. Taa katika baadhi ya ushoroba hazizimwi , lakini Doroshenko na wenzake daima hubeba tochi.
Njia zingine ni nyembamba kiasi kwamba wanapaswa wanatembea wakiwa wameinama.
Vyumba na shoroba zote zimewekwa alama, lakini unahitaji kujua njia vizuri ili usipotee kwenye (maze) njia nyingi za kupitia kwenye kiwanda cha nyuklia .
Pia zina ramani zinazoonyesha maeneo ambayo yana kiwango cha juu zaidi cha mionzi.
"Hapa, wanasayansi wote wanajua ni wapi wanaweza kufanya kazi na wapi hawawezi," anaelezea Doroshenko.

Chanzo cha picha, Getty Images
Eneo hilo limejaa mirija yenye maji ya mionzi na miundo hatari ya *corium*—dutu iliyotokea wakati mafuta ya nyuklia yalipochanganyika na sehemu za msingi wa mtambo huo kutokana na joto kali lililofikia maelfu ya nyuzi joto Selsiasi.
Kama lava, dutu hii ilitiririka na kupenya katikati ya vifusi, ikitengeneza maumbo ya ajabu. Mojawapo ya maumbo hayo ya kipekee inajulikana kama "mguu wa tembo."

Chanzo cha picha, Getty Images
Maeneo yasiofikika
Kulingana na shirika la kimataifa la Nishati ya Atomiki kuna takribani tani 200 za mafuta ya nyuklia According to the International Atomic Energy Agency, there are approximately 200 tonnes of yaliyosalia kwenye Kitengo cha 4.
Urejeshaji wa nyenzo hizi zenye mionzi mingi unatarajiwa kuchukua takriban miaka 40.
Jambo hilo lote limefunikwa na sarcophagus, yenyewe iliyozungukwa na "Kidhibiti Kipya cha Usalama," kuba ya chuma ndefu zaidi kuliko Sanamu ya Uhuru, iliyoundwa ili kuziba reactor nambari 4 kwa miaka 100 na kulinda ulimwengu kutokana na mionzi ya Chernobyl.
Sehemu kubwa ya mafuta haya ya nyuklia iko katika maeneo ambayo hayafikiki kwa Doroshenko na wenzake.

Baada ya mlipuko wa 1986, Kitengo cha 4 kilifunikwa na kiasi kikubwa cha saruji ili kuzuia uvujaji wa mionzi.
"Ikiwa tungeweza kuchukua sampuli kutoka kwa kinu kilichoharibiwa, tunaweza kuamua kwa usahihi kiwango chake cha hatari ya nyuklia," anaelezea Doroshenko.
"Lakini imefunikwa kwa saruji na haiwezi kufikiwa. Ndiyo maana tunachukua vipimo, ili kuelewa michakato inayofanyika ndani ya nishati ya nyuklia."

Chanzo cha picha, Getty Images
Taadhari unapoingi akwenye kinu
Ili kuingia kwenye kinu cha nyuklia, Doroshenko huvalia mavazi maalum ya kinga, ikiwa ni pamoja na mikono, viatu, na kipumuaji cha FFP2 chenye vali. Katika baadhi ya maeneo membamba ambapo analazimika kupitia kifusi, huvaa suti maalum ya plastiki inayonyumbulika.
Unapotoka, lazima upitie vituo kadhaa vya ukaguzi na "eneo chafu" ambapo unavua nguo zako, ambazo husafishwa au kuharibiwa moja kwa moja ikiwa haiwezekani kuondoa mionzi.
Kinachofuata ni kuoga kwa makini ili kuhakikisha mwili wako hauna chembe zenye mionzi.

Chanzo cha picha, Doroshenko
Doroshenko anapenda kazi yake.
Anasema kuenda hadi Kitengo cha 4 cha mtambo huo kunamweka katika hali ya "furaha", hisia anazozingatia kulinganishwa na hisia alizozipata wakati wa kupanda Everest.
Hata hivyo, anasisitiza kuwa jambo muhimu zaidi ni kudumisha udhibiti.
"Jambo muhimu zaidi sio kuogopa, kwa sababu hofu huongeza hatari ya kufanya makosa."

Chanzo cha picha, Getty Images
"Sehemu hii imeshuhudia na matukio ya kutisha ambayo yamewafanya baadhi ya watu kupaita kuzimu, lakini hakutishi kama vile watu wanavyojaribu kuwafanya watu waamini.
"Unapokuwa huko, unagundua kuwa ni muundo ulioundwa na mwanadamu. Unaelewa kuwa nafasi hii inahitaji ufuatiliaji na udhibiti wa mara kwa mara."
"Ikiwa watu kama sisi wataacha kwenda huko, mchakato usioweza kudhibitiwa utaanza, na hiyo ni hatari," anasema.

Chanzo cha picha, Getty Images
"Chernobyl haipaswi kusahaulika"
Mara moja kwa mwaka, Doroshenko hupitia uchunguzi wa lazima wa matibabu na, wakati wa likizo yake, daima anajaribu kwenda baharini.
"Nitaendelea kushuka kwenye kinu cha nyuklia kwa muda mrefu kadiri ya uwezo wangu," alisema.
"Sijajiwekea mipaka yoyote. Ikiwa ningeona kizazi chenye uwezo wa kuchukua nafasi yangu, ningekuwa tayari kufikiria kustaafu. Lakini kwa sasa, sifikirii juu ya hilo."
Kwa ajili yake, jambo muhimu zaidi ni kwamba watu kukumbuka changamoto zinazokabili Chernobyl: zenye mionzi kutoka kwa taka ya mafuta ya nyuklia na kudumisha udhibiti wa vifaa.
"Ni kazi ngumu," alisema.
"Chernobyl haipaswi kusahaulika."
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi












