Kwa nini Iran iliamua kuishambulia Israel?

Chanzo cha picha, Wisam Hashlamoun/Anadolu via Getty Images
Baada ya miezi kadhaa ya usitishaji mapigano uliokumbwa na visa vya Iran na Marekani kushambuliana hapa na pale, makombora ya balistiki ya Iran yalirushwa tena Jumapili jioni kuelekea maeneo kadhaa nchini Israel.
Tukio ambalo, kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa kijeshi nchini Iran, lilikuwa hatua ya " kulipiza kisasi mashambulizi ya Israel dhidi ya vitongoji vya Beirut."
Ingawa maafisa wa Iran walidai tangu mwanzo wa usitishaji vita kwamba mpango huo mpya wa maelewano utajumuisha pia Lebanon, Israel haikuwahi kuzingatia kipengele hiki, na katika kipindi hiki, ilishambulia maeneo kadhaa nchini humo.
Wiki iliyopita, Israel ilitangaza kuwa itafanya mashambulizi makubwa katika vitongoji vya kusini mwa Beirut. Lakini Tehran ilitishia kuchukua hatua operesheni hiyo ikitekelezwa. Na hapo ndipo Rais wa Marekani Donald Trump alipoitaka Israel kutoishambulia Lebanon hadharani.
Trump aliandika katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa Truth Social kwamba amewahakikishia Israel na maafisa wa Hezbollah kupitia mawasiliano ya simu kwamba hakuna shambulio lolote litakalofanywa na pande zote mbili.
Tukio ambalo baadhi ya vyombo vya habari na wachambuzi walio karibu na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wamelitafsiri kuwa ni ishara ya mafanikio ya tishio la Tehran.
Lakini hali ya utulivu ulidumu kwa siku chache kabla ya Jeshi la Israel kutangaza Jumapili mchana kwamba limeshambulia maeneo kadhaa viungani mwa Beirut. Ingawa haijabainika ni watu wangapi waliouawa au kujeruhiwa katika shambulio hilo, mamlaka nchini Iran ilijibu hatua hiyo kurusha msururu wa makombora kuelekea Israel.
Awali Mohammad Baqer Qalibaf aliandika kwenye akaunti yake ya X-Net: "Hawazingatii makubaliano ya usitishaji vita wala hawatilii maanani mazungumzo ya amani. Kwa kuendelea kutekeleza kizuizi cha majini na ukiukaji wa makubaliano kuhusu Lebanon, walionyesha kwamba wanaelewa tu lugha ya kutumia nguvu."
Tangu wakati huo, baadhi ya waangalizi wametabiri kuwa Iran huenda ikaamua kujibu hatua hiyo ya Israel.

Chanzo cha picha, Hamed Malekpour - ICANA News Agency via Getty Images
Kwanini Iran imeishambulia Israel?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Tangu kuuawa kwa Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, baadhi ya viongozi wakuu katika serikali ya Iran wameonekana kutafakari upya mafundisho ya kijeshi na usalama wa nchi hiyo.
Baadhi ya wachambuzi wanaamini kwamba misimamo ya Tehran baada ya vita vya siku 12 ikifuatiwa na vile vya siku 40 vimefichua dalili ya mabadiliko haya. Katika miaka ya mwisho ya serikali ya Ali Khamenei, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilijaribu kujiepusha na mgogoro wa moja kwa moja liicha ya vitisho na mivutano inayoongezeka, mtazamo huu naonekana kubadilika kwa kiwango fulani baada ya vita vya hivi karibuni.
Baada ya kuuawa Ali Khamenei, Iran ilianzisha mashambulizi dhidi ya Israel na mataifa ya kadhaa ya Ghuba kadhaa ili kukabiliana na mashambulizi ya Israel na Marekani katika eneo hilo.
Kauli za Mohammad Baqer Qalibaf pia zinaonyesha sehemu ya simulizi ambayo polepole imechukua sehemu kubwa katika mazungumzo ya watoa maamuzi katika serikali ya Jamhuri ya Kiislamu katika miaka ya hivi karibuni: ambapo spika wa bunge anasema: "Wanaelewa tu lugha ya nguvu," mfano ambao unatambuliwa na baadhi ya taasisi na watu wenye ushawishi ndani ya serikali kama njia pekee ya kukabiliana na utawala wa Donald Trump.

Chanzo cha picha, Morteza Nikoubazl/NurPhoto via Getty Images
"Ili kuepuka vita visivyo na mwisho, lazima upigane''
Baadhi ya wate wenye ushawishi mkubwa nchini Iran wamekubaliana kwamba ili kuzuia vita visivyo na mwisho, ni lazima mtu aonyeshe uwezo wake kabla ya kufikia makabiliano. Hii inamaanisha kuwa pande zote mbili zinatoa ujumbe kwamba ''tuko tayari kwa lolote na hawaogopi'', kwa matumaini kwamba mwishowe upande mmoja utarudi nyuma.
Dalili za mtazamo huu pia zimejitokeza katika taarifa za maafisa wa kijeshi na ulinzi wa Iran. Reza Talaeinik, msemaji wa Wizara ya Ulinzi, alisema Mei 12: "Tishio lolote jipya, uchokozi, au adui bila shaka utakabiliwa na jibu la haraka, la mwisho, na la kujutia upande kwao." Pia alisema kwamba "kushindwa kwa adui mara kwa mara kwenye uwanja wa vita" kunatabirika.
Pia Hassan Hassanzadeh, kamanda wa Walinzi wa Mapinduzi ya Mohammad Rasoolullah huko Tehran, alisema tarehe 13 Mei mwaka huu baada ya zoezi la siku tano: "Tuko tayari kutekeleza operesheni yoyote wakati wowote na katika muda wowote kwa muda mfupi iwezekanavyo." Alisema kuwa lengo la zoezi hili lilikuwa ni kuimarisha uwezo wa kupambana ili kukabiliana na "adui wa Marekani na Israel."
Hata hivyo haijabainika ni kwa kiasi gani mtazamo huo umepata ufanisi katika sekta zote za serikali ya Iran, hasa wakati huu ambapo juhudi za kidiplomasia za kufikia makubaliano na Marekani zikiendelea.
Kwa kuzingatia kwamba Iran ilipata pigo kubwa wakati wa vita vya siku 40, baadhi ya wachunguzi waliamini kuwa Tehran haikuwa na hamu ya kuanzisha tena vita vikubwa; hata hivyo, kwa kufanya mashambulizi dhidi ya Israel, nchi hiyoinatuma ujumbe kwa hasimu wake kwamba haiogopi vita vingine ilikuwarejesha kwenye suala lililopo mezani.
Aidha, matamshi ya Donald Trump katika wiki za hivi karibuni na msisitizo wake wa mara kwa mara kwamba anatafuta mapatano na Iran yanaleta taswira nyingine katika mzozo huu. Wachambuzi wanaamini kuwa, huenda baadhi ya maafisa wa Iran wamezitafsiri kauli za hivi karibuni za Donald Trump kuwa ni ishara ya kutaka kuepusha vita vikubwa zaidi na hivyo kutoa furasa kwao kukariri matakwa yao.
Donald Trump amesema mara kwa mara katika wiki za hivi karibuni kwamba bado ana nia ya kufikia makubaliano na Iran, na alisisitiza, hili katika mahojiano na NBC: "Nadhani naweza kusubiri kwa muda wanaotaka."
Uamuzi mgumu wa Netanyahu

Chanzo cha picha, Ilia YEFIMOVICH / AFP via Getty Images
Dakika chache baada ya Iran kuanzisha mashambulizi yake dhidi ya Israel, Rais wa Marekani Donald Trump, katika mahojiano na Fox News, aliitaka Israel kutojibu hatua ya Iran.
Katika mfululizo wa mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari, pia alimkosoa Benjamin Netanyahu kwa kuishambulia Lebanon, shambulio ambalo Bw.Trump alisisitiza kuwa lilitekelezwa bila uratibu wake.
Rais wa Marekani pia aliongeza kuwa atampigia simu Netanyahu na kumwambia kwamba hatakiwi kujibu mashambulizi ya Iran. Katika mahojiano na gazeti la Financial Times, pia alisema: "Mimi ndiye maamuzi, sio Netanyahu; Israel haina budi kufikia makubaliano na Iran."
Lakini saa chache baada ya Trump kuwasiliana na Netanyahu kwa njia ya simu, ndege za kivita za Israel zilishambulia maeneo mbalimbali nchini Iran. Hii iliongeza zaidi mvutano na hatari ya kuzuka tena kwa vita vya kikanda. Lakini kabla ya kutathmini uamuzi wa Netanyahu, kauli za rais wa Marekani kuhusiana na upinzani wake dhidi ya Israel zinastahili kuzingatiwa.
Msururu wa mahojiano yake na vyombo mbalimbali vya habari Jumapili usiku unaonyesha wazi kwamba anapinga mashambulizi ya Israel. Hata hivyo baadhi ya wachambuzi wametilia shaka hatua ya Trump na kuitaja kuwa mbini za udanganyifu Marekani na Israel. Wanasema ni mchezo anaucheza Trump hadharani mbele ya waandishi wa habari lakini nyuma ya pazia inampa Netanyahu idhini ya kuishambulia Iran.
Kabla ya Israel kushambulia Iran, wachambuzi walikuwa wametabiri kwamba Netanyahu bila shaka atajibu mashambulizi ya makombora ya Iran na kwamba hilo halingeepukika.
Hatua ya haraka ya Israel kujibu mashambulizi ya Iran inaashiria kuwa huenda Netanyahu alipima athari ya kisiasa na kiusalama ya kutojibu zaidi ya hatari ya kuongezeka kwa mivutano, kwa sababu kama angeamua kufanya vile rais wa Marekani alitaka na kutojibu mashambulizi ya Iran, angekabiliwa na wimbi la mashambulizi dhidi ya Israel, ndani na nje ya baraza la mawaziri.
Dakika chache baada ya mashambulizi ya makombora ya Iran, Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel Itamar Ben-Gavana aliandika kwenye mtandao wake Twitter: "Lazima tuteiketeze Tehran usiku wa leo."
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel Naftali Bennett, mwanasiasa anayempinga Benjamin Netanyahu, pia aliandikao: "Kujidhibiti kunamaanisha kumwaga bure damu ya raia wetu." Bw. Bennett pia alisisitiza haja ya kujibu mashambulizi hayo ya Iran, akiandika: "Huu ni wakati wa kujiuliza maswali magumu. Je, Israel ni nchi huru iliyo na uwezo wa kujilinda?"















