Tetesi za soka Ulaya: Rodri kutua Madrid

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Real Madrid ina imani kubwa ya kufanikisha usajili wa kiungo wa Hispania Rodri, mwenye umri wa miaka 30, kutoka Manchester City kwa ada inayokadiriwa kufikia euro milioni 40-50 (£34m-£43m). Rodri amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na City, huku makubaliano yakitarajiwa kukamilika baada ya mkutano wa leo Alhamisi. (AS)

Inter Milan inaweza kufufua jitihada za kumsajili kiungo wa England Curtis Jones, mwenye umri wa miaka 25, kutoka Liverpool. Wakati huo huo, ujio wa beki wa kati wa England John Stones, mwenye umri wa miaka 32, kwa uhamisho wa bure unaweza kuzima matumaini ya beki wa Argentina Cristian Romero, mwenye umri wa miaka 28, kujiunga na klabu hiyo kutoka Tottenham. (Gazzetta dello Sport)

Juventus imefikia makubaliano na Paris St-Germain ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Randal Kolo Muani kwa mkopo wenye kipengele cha lazima cha kumnunua. Thamani ya dili hilo inaweza kufikia euro milioni 50 (£43m) (Sky Sports Italia)

Brentford ipo karibu kukamilisha usajili wa kiungo wa Mali Mamadou Sangare, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Lens kuchukua nafasi ya Jordan Henderson. (Evening Standard)

Aston Villa imekataliwa ofa ya euro milioni 30 (£26m) kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazil Allan, mwenye umri wa miaka 22, anayekipiga katika Palmeiras. (ESPN)

Hull City ipo katika mazungumzo na Aston Villa kuhusu usajili wa moja kwa moja wa winga wa Jamaica Leon Bailey, mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)

Fulham inakaribia kuwasajili wachezaji wawili wa Hispania kutoka Real Madrid - kiungo mshambuliaji Cesar Palacios, mwenye umri wa miaka 21, na mshambuliaji Gonzalo Garcia, mwenye umri wa miaka 22. Wawili hao walifanya kazi chini ya kocha mpya wa Fulham Alvaro Arbeloa wakati akiwa Real Madrid msimu uliopita. (Athletic)

Nottingham Forest imekataliwa ofa ya euro milioni 20 kwa ajili ya mchezaji wa kimataifa wa Israel Anan Khalaili, mwenye umri wa miaka 21, ambaye anaweza kucheza kama beki wa kulia au winga, kutoka klabu ya Ubelgiji Royale Union Saint-Gilloise. (Athletic)

Manchester United iko tayari kuwauza kipa wa Jamhuri ya Czech Radek Vitek, mwenye umri wa miaka 22, na beki wa England Harry Amass, mwenye umri wa miaka 19. Pia viungo wa England Toby Collyer, mwenye umri wa miaka 22, na Dan Gore, mwenye umri wa miaka 21, ambao hawapo kwenye mipango ya klabu hiyo. (Mail)

Nottingham Forest ipo mbioni kumsajili kiungo wa Ureno Gustavo Sa, mwenye umri wa miaka 21, kutoka Famalicao, kabla ya kumpeleka kwa mkopo Olympiacos ya Ugiriki. (Athletic)

Mazungumzo kati ya Crystal Palace na Augsburg kuhusu usajili wa beki wa Ufaransa Chrislain Matsima, mwenye umri wa miaka 24, yamesimama, huku Palace ikianza kuangalia wachezaji wengine. (Standard)