Lissu: Waeleze majajji nani aliyeamua huo mkutano ufanyike

Brenda ni shahidi mwengine wa upande wa Tundu Lissu
Lissu: Nje ya hizi nafasi za kichama wewe ni nani
Brenda: Mimi nimesomea Bachelor of science in Accounting Gloucestershire University nchni Uingereza kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2013
Lissu: Waeleze majaji Tuzo au awards uliyoipata baada ya kusoma huko
Brenda: Nilipata Cheti baada ya kuhitimu
Lissu: Waeleze majaji utaalamu wako mwingine kama upo
Brenda: Hapana hakuna
Lissu: Waeleze majaji uzoefu wako wa kazi za kitaaluma nje ya kazi za kisiasa
Brenda: Kwa mwaka mmoja baada ya kuhitimu nilifanya kazi kwa mwaka mmoja na baadae nikaanza kufanya biashara za kawaida
Lissu: Waeleze majaji ulifanya kazi gani wapi na mwaka gani
Brenda: Niliajiriwa kama accountant TAZ Cars nilifanya kwa mwaka mmoja nikaanza kufanya biashara Kariakoo
Lissu: Ulifanya kazi kwenye hiyo kampuni toka lini hadi lini
Brenda: Nilipohitimu mwaka 2013 niliajiriwa mpaka mwaka 2015 na baada ya hapo nikaanza kufanya biashara ya nywele na urembo wa wanawake Kariakoo na baadaye nikaanza kuuza vifaa vya umeme
Lissu: Ukisema uliuza urembo una maaana gani?
Brenda: Nilikuwa nauza vifaa vya urembo
Lissu: Sasa shahidi baada ya kutupa historia yako kwa ufupi naomba tuzungumzie kesi ambayo unaitolea ushahidi leo hii. Swali langu la kwanza kuhusiana na hii kesi waeleze majaji ufahamu wako juu ya mkutano wa tarehe tatu April 2025
Brenda: Waheshimiwa majaji Chama kilialika watia nia makao makuu ya chama mikocheni kuja kuzungumzia kuhusiana na msimamo wa ‘No reforms no election’
Lissu: Waeleeze majaji hao watia nia ni watu gani
Brenda: Ni wale waliokuwa na nia kugombea chaguzi za kiserikali 2025
Lissu: Waeleze majaji hiyo uliyokuja kuzungumzia ‘No reforms no election ni nini
Brenda: Ni msimamo wa chama ulioelekeza bila mabadiliko hakuna uchaguzi mabadiliko ya sheria za kiuchaguzi
Lissu: Waeleze majajji nani aliyeamua huo mkutano ufanyike
Brenda: Ni katibu mkuu wa chama na sekretarieti
Lissu: Katibu mkuu ni nani?
Brenda: Waheshimiwa majaji katibu mkuu anaitwa John Mnyika
Lissu: Unaposema sekretarieti una maana gani shahidi
Brenda: Ni chombo cha utekelezaji wa kazi za chama za kila siku
Lissu: Hiki chombo kina wajumuisha wakina nani?
Brenda: Waheshimiwa majaji hiki chombo kinaundwa na katibu mkuu na manaibu wake wawili wa bara na Zanzibar Mkurugenzi wa chama
Lissu: Hao manaibu katibu hawana majina
Brenda: Mmoja anaitwa Amani Golugwa bara na wa Zanzibar anaitwa Ally Ibrahim
Wakurgenzi ni Brenda Rupia mkurugenzi mawasiliano na uenezi, John Kitoka mkurugenzi mambo ya nje, Mkurugenzi wa Fedha Tito Kitalika, Mkurugenzi wa operesheni na uchaguzi John Pambalu, Mtaalamu wa rasilimali Lenard Magere, Makatibu wa mabaraza , Baraza la wazee Hellen Kayanza, Baraza la wanawake Pamela Maasai, Baraza la vijana Dua Lyamzito, Mkurugenzi wa sheria Gaston Galubindi.
Lissu: Waeleze majaji huo mkutano wa sekretarieti ulifanyika lini?
Brenda: Sikumbuki tarehe ya kikao tulichofanya ili kuitisha huo mkutano
Lissu: Sasa waeleze waheshimiwa majaji kikao hicho kiliamua nini kifanyike
Brenda: Waheshimiwa majaji kikao hicho kiliamua kwamba tutoe taarifa kwa watia nia kwenye huo mkutano na kwamba Chadema itakuwa na watia nia kwenye huo mkutano
Lissu: Baada ya kuamua watia nia wafahamishe na umma ufahmishwe kitu gani kilifanyika
Brenda: Mkurugenzi wa mawasiliano aliandika ujumbe kwa umma tarehe 27/03/2025 kuujulisha umma kutakuwa na mkutano na watia nia tarehe tatu April na kuwataka watia nia wafike ofisi za chama kwa ajili ya mkutano huo na chama.
Lissu: Nini kilifuata
Brenda: Tuliweka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii baada ya kuwa nimeandika kwa kurugenzi yangu ya mawasiliano ambayo ilitoa taarifa juu ya mkutano huo kwa vyombo vya habari na nikavialika
Lissu: Naomba urudie tena
Brenda: Niliandika barua nikaweka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii za Chama, Kisha nikaalika vyombo vya habari
Lissu: Sasa mimi nimeshitakiwa na nimekuwa gerezani nikituhumiwa mimi ndiye niliyealika vyombo vya Habari, wewe unasemaje?
Brenda: Waheshimiwa majaji Mheshimiwa Tundu Lissu sio yeye aliyeandaa mkutano na watia nia wala kualika vyombo vya habari
Lissu: Waeleze majaji kwenye mwaliko wa waandishi wa habari iwapo kulikuwa na maelekezo yoyote waje na nini na waje wafanye kazi yao vipi
Brenda: Tunapowaalika waandishi wa habari hatuwapi maelekezo yoyotewanakuja kufanya kazi yao kwa utaalamu wao, na tuliwaalika waje wachukue taarifa ya watia nia na chama
Lissu: Waeleze majaji siku ya mkutano watu gani walihudhuria mkutano huo
Brenda: Waheshimiwa majaji watia nia walihudhuria, wajumbe wa sekretarieti pamoja na viongozi wakuu wa Chama
Lissu: Viongozi wakuu wa chama ni akina nani
Brenda: Viongozi wakuu wa chama ni Manaibu makatibu wakuu wawili Aman Golugwa na Ally Ibrahim, Makamu mwenyekiti Zanzibar Said Mzee Makamu, mwenyekiti Bara Mheshimiwa John Heche na Mwenyekiti Taifa Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu na katibu mkuu wa Chama Mheshimiwa John Mnyika.
Lissu: Watu gani wengine walikuepo?
Brenda: Walikuepo watia nia wa sekretarieti pamoja na waandishi wa habari
Lissu: Ulikuwa na wastani wa watu wangapi?
Brenda: Takribani watu 250
Lissu: Waeleze majaji kimahususi kuhusiana na waandishi wa habari waliokuja ni wa vyombo gani vya habari
Brenda: Waandishi waliokuja ni pamoja na Chanzo TV Mwanzo TV, Jambo TV, ITV na vyombo vingine vya online ikiwemo Mwananchi, hao ndio ninaowakumbuka
Lissu: Walikuja vipi?
Brenda: Waheshimiwa majaji walikuja na kamera na vipaza sauti na wengine kalamu na karatasi
Lissu: Sasa ushahidi umeletwa mahakamani, kati ya hao waandishi wa habari waliokuja, wapo waliorusha matangazo ya mkutano huo moja kwa moja waeleze majaji moja kwa moja
Brenda: Ni ngumu kesema kama walirusha au hawakurusha sababu kuna wanaorekodi na kurusha baadaye na kuna ambao hawatarusha kabisa
Lissu: Kuna taarifa kwamba Jambo TV walirusha Taarifa hiyo moja kwa moja, wewe unasemaje?
Brenda: Waheshimiwa majaji ni ngumu kusema sababu hatuwapangii namna ya kufanya kazi
Lissu: Wewe ulikuwepo kwenye huo mkutano uliona wakifanyaje kazi?
Brenda: Waheshimiwa majaji, waandishi walikuwepo ila ni ngumu kusema kama walirusha matangazo moja kwa moja au la au hata kama walirekodi sababu walikuwa tu kwenye huo mkutano
Lissu: Kwa kuwa mimi ndio mshitakiwa waeleze majaji mimi nilifanya nini kwenye mkutano huo
Brenda: Mwenyekiti alikuwa mzungumzaji pamoja viongozi wengine wa chama
Lissu: Nilikuwa mzungumzaji wa aina gani?
Brenda: Hapana ulikuwa mzungumzaji mwalikwa na ulitoa hotuba kama mwenyekiti wa chama na ndio alikuwa mzungumzaji mkuu
Lissu: Waeleze majaji kitu kingine chochote ulichokiona mwenyekiti akifanya zaidi ya kuwa mzungumzaji mkuu
Brenda: Sikuona kitu kingine chochote mwenyekiti alichokifanya zaidi ya kuwa mzungumzaji mkuu
Lissu: Ushahdi uliopo unasema mimi ndiye niliyetayarisha hayo matangazo na kuyaweka mitandaoni hususan jambo tv wewe unasemaje?
Brenda: Waheshimiwa majaji hayo yatakuwa mashitaka ya uongo na wala sio mfanyakazi wa jambo tv hayo ni mashitaka ya uongo na wala alikuwa hafahamu kama Jambo tv watakuepo kwenye huo mkutano
Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji Nzengelei waheshimiwa majaji tunaona muda umekwisha tunaomba muongozo wa mahakama kama shauri linaweza kuahirishwa
Jaji: Tuendelee kidogo
Lissu: Ahsante waheshimiwa nimalizie hili. Shahidi swali langu lilikuwa mwenyekiti hakuwa anajua juu ya uwepo wa jambo TV waeleze majaji mwenyekiti kufahamu kama anajua waandishi wa habari walikuwa wamealikwa
Brenda: Sinadhani kama alikuwa anafahamu, sababu ni kazi yangu mimi na kurugenzi ya mawasiliano
Lissu: Swali langu la mwisho kwa leo nani ni mmiliki wa hayo matangazo au hiyo Taarifa.
Brenda: Ni Mmiliki wa chombo husika
Lissu: Waeleze majaji kuhusu Taarifa iliopeperushwa na Jambo tv April tatu mwaka jana
Brenda: Waheshimiwa majaji mmiliki wa taarifa ya Jambo TV ni jambo TV wenyewe au mkurugenzi wa Jambo TV
Jaji: Shauri linaahirishwa mpaka kesho saa tatu asubuhi








