Meli ya mafuta yapita Hormuz baada ya makubaliano ya kumaliza vita kutangazwa
BBC Verify imekuwa ikichunguza data ya ufuatiliaji wa meli ambayo inaonekana kuonyesha kwamba meli moja ya mafuta imevuka Mlango-Bahari wa Hormuz kufuatia tangazo la Rais Donald Trump la kufikiwa kwa makubaliano kati ya Marekani na Iran.
Kulingana tovuti ya MarineTraffic, meli ya mafuta yenye bendera ya Malta Disha iliondoka kwenye bandari ya Ras Laffan nchini Qatar tarehe 13 Juni ikiwa na mizigo.
Meli nyingine, yenye bendera ya Panama ya MDL Kamran, iliondoka Bandar Imam Khomeini nchini Iran tarehe 11 Juni na kuvuka lango hilo la bahari hapo jana.
Vifuatiliaji vya eneo lake vilizimwa wakati vikipita kwenye njia ya maji na vilianza tena kusambaza baada ya kupita mkondo huo.
Meli hiyo inaelekea bandari ya Shinas nchini Oman.
























