Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Man City yajiandaa kwa ofa ya Rodri kutoka Madrid
Paris St-Germain hawana mpango wa kumsajili kiungo wa kati raia wa Uhispania, Rodri, mshindi wa Kombe la Dunia kutoka Manchester City. (Sky Sports)
Hata hivyo, City wanajiandaa kwa ofa kutoka kwa miamba wa Uhispania, Real Madrid kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 lakini wana matumaini kwamba atasaini mkataba mpya. (Guardian)
Leeds United wamejiandaa kukubali mkataba wa pauni milioni 40 ili kumsajili kipa wa Uingereza, James Trafford mwenye umri wa miaka 23 kutoka Manchester City. (Athletic)
Manchester United wameingia katika mazungumzo ili kumpeleka mshambuliaji wa Uholanzi, Joshua Zirkzee, 25, kwa mkopo wa msimu mzima Juventus katika makubaliano ambayo yanajumuisha chaguo la kumnunua kwa pauni milioni 30. (Sun)
Paris St-Germain wanavutiwa na Zion Suzuki wa Parma, kipa wa Japan mwenye umri wa miaka 23 ambaye amehusishwa na Aston Villa na Juventus. (Sky Sport)
Crystal Palace wamefikia makubaliano kuhusu masharti binafsi na beki wa kati wa Brest, Mfaransa, Raphael Le Guen, mwenye umri wa miaka 19. (L'Equipe)
Ibrahim Mbaye wa Paris St-Germain amepewa ofa na Liverpool na Manchester City baada ya mawakala wake kuweka wazi kuwa mshambuliaji huyo wa Senegal, 18, hatajiunga na Aston Villa msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Real Madrid itafanya mazungumzo zaidi na wawakilishi wa Vinicius Jr, wakitarajia kupata makubaliano kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu, huku Arsenal ikimtaka winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 26. ( Sky Sports)
Real Madrid wametoa ofa ya pili yenye thamani ya kati ya pauni milioni 94 na 98 kwa winga wa Ivory Coast, Yan Diomande lakini mazungumzo zaidi yanahitajika ili kukidhi mahitaji ya RB Leipzig kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye pia alikuwa shabaha ya Liverpool. (Sky Sport)
Sevilla wako tayari kumuuza Ruben Vargas, 22, kwa euro milioni 20 (pauni milioni 17) huku Brighton, Newcastle na Aston Villa zikiwa miongoni mwa vilabu vya Ligi Kuu England vinavyomtaka winga huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 27. ( Mundo Deportivo)
Sunderland wamekubaliana na masharti binafsi ya beki wa kushoto wa Toulouse na Ufaransa chini ya umri wa miaka 21, Dayann Methalie, 20. ( RMC Sport)
Mchezaji wa kimataifa wa Fulham, Sasa Lukic raia wa Serbia mwenye umri wa miaka 29, ni mmoja wa wachezaji kadhaa wa kiungo wanaotakiwa na timu ya Ipswich Town msimu huu wa joto. ( Sky Sports)